
The Tower of Babel (Genesis 11: 1-9)
Swahili
- Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
- Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi
tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
- Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto.
Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
- Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake
kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni
pa nchi yote.
- Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
- Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao
ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa
neno wanalokusudia kulifanya.
- Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane
maneno wao kwa wao.
- Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote;
wakaacha kuujenga ule mji.
- Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana
alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya
waende usoni pa nchi yote.
Information about the Swahili language
Swahili language learning materials
Tower of Babel in Bantu languages
Bemba,
Beti,
Chichewa,
Dawida,
Kamba,
Kinyarwanda,
Kirundi,
Kwanyama,
Lingala,
Luba-Katanga,
Luganda,
Luragooli,
Ndebele,
Ndonga,
Northern Sotho,
Sena,
Shona,
Southern Sotho,
Swahili,
Tetela,
Tonga,
Tsonga,
Tswana,
Tumbuka,
Venda,
Xhosa,
Zulu
Other Tower of Babel translations
By language |
By language family
Learn Chinese Characters with the Omniglot Chinese app